عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: إِنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ:
«إِذَا شَرِبَ الْكَلْبُ فِي إِنَاءِ أَحَدِكُمْ فَلْيَغْسِلْهُ سَبْعًا».
ولمسلم: « أولاهُنَّ بالتُراب».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 172]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 172]
Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake chombo hicho kioshwe mara saba ikiwa mbwa ataingiza ulimi wake ndani yake, mara ya kwanza iwe kwa mchanga, ili yaje maji baada yake, hivyo usafi kamili utakuwa umepatikana kutokana na najisi yake na madhara yake.