عن أبِي هريرة رضي اللَّه عنه: سمعتُ النبِيّ صلى الله عليه وسلم يقول:
«الفِطْرَةُ خمسٌ: الخِتَانُ والاستحدادُ وقصُّ الشَّارِبِ وتقليمُ الأظفارِ وَنَتْفُ الآبَاطِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5891]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5891]
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mambo matano katika dini ya Uislamu na sunna ya Mitume:
La kwanza: Kutairi, nako ni kukata ngozi iliyozidi juu ya kichwa cha dhakari kwa mwanaume, na kukata kingozi katika tupu ya mwanamke juu ya malaha palipo tundu la uke.
La pili: Kunyoa sehemu za siri, nako ni kunyoa nywele za kinena zinazozunguka tupu ya mbele.
La tatu: Kupunguza masharubu, nako ni kupunguza kilichoota juu ya mdomo wa juu wa mwanaume mpaka mdomo uonekane wazi.
La nne: Kupunguza kucha.
La tano: Kunyofoa nywele za kwapa.