عَنِ شُرَيْحٍ بنِ هانِئٍ قَالَ:
سَأَلْتُ عَائِشَةَ، قُلْتُ: بِأَيِّ شَيْءٍ كَانَ يَبْدَأُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا دَخَلَ بَيْتَهُ؟ قَالَتْ: بِالسِّوَاكِ.
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 253]
المزيــد ...
Kutoka kwa Shuraihi bin Hanii amesema:
Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 253]
Ilikuwa katika muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuanza na mswaki anapoingia nyumbani kwake wakati wowote, usiku au mchana.