عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ:
قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَقُولُ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ: أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي، وَأَنَا مَعَهُ حِينَ يَذْكُرُنِي، فَإِنْ ذَكَرَنِي فِي نَفْسِهِ ذَكَرْتُهُ فِي نَفْسِي، وَإِنْ ذَكَرَنِي فِي مَلَإٍ ذَكَرْتُهُ فِي مَلَإٍ خَيْرٍ مِنْهُ، وَإِنِ اقْتَرَبَ إِلَيَّ شِبْرًا، تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعًا، وَإِنِ اقْتَرَبَ إِلَيَّ ذِرَاعًا، اقْتَرَبْتُ إِلَيْهِ بَاعًا، وَإِنْ أَتَانِي يَمْشِي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2675]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: Mimi nipo katika dhana ya mja wangu kwangu, na Mimi nipo naye wakati anaponitaja, atakaponitaja ndani ya nafsi yake nami nitamtaja ndani ya nafsi yangu, na akinitaja katika umati nami nitamtaja katika umati bora kuliko huo, na akisogea kwangu shibri (futi) moja na mimi ninasogea karibu naye kwa mita nzima, na akisogea kwangu kwa mita moja mimi ninasogea kwake kwa zaidi ya mita moja (Baa'a) na akinijia kwa kutembea basi mimi nitamjia kwa mchakamchaka"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2675]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
Mimi nipo katika dhana ya mja wangu kwangu, nitampeleka mja wangu kulingana na dhana yake kwangu na hii ni kwa kutaraji mazuri na kutaraji msamaha, na nitamfanyia yote anayoyataraji kutoka kwangu katika mambo ya kheri au mengineyo; na mimi niko pamoja naye kwa kumhurumia na kumuwezesha na kumuongoza na kumlea na kumuunga mkono pindi anaponitaja.
Akinitaja ndani ya nafsi yake akiwa peke yake amejitenga kwa kunisabihi na kunitukuza au kwa kinginecho; basi nami nitamtaja ndani ya nafsi yangu.
Na akinitaja katika kundi la watu; basi nami nitamtaja katika kundi kubwa na zuri kuliko hilo.
Na atakayesogea kwa Mwenyezi Mungu kwa kiwango cha shibri (futi) moja basi Mwenyezi Mungu humzidishia na kuzidi kujiweka karibu zaidi kwa kiasi cha dhiraa (mita).
Na akijiweka karibu naye kwa kiasi cha dhiraa (mita) anajiweka naye kwa kiasi cha zaidi ya mita moja (Baa'a).
Na akija kwa Mwenyezi Mungu akiwa anatembea Yeye anamjia kwa mchakamchaka.
Mja atakapojiweka karibu na Mola wake Mlezi kwa kumtii na kuelekea kwake, basi Mola Mlezi Mtukufu humzidishia ukaribu ikiwa ni malipo kulingana na amali yake.
Kila unapozidi kukamilika uja (utumwa) wa muumini kwa Mola wake Mlezi Mwenyezi Mungu Mtukufu hujiweka karibu naye, hivyo, kipawa cha Mwenyezi Mungu na thawabu zake ni nyingi kuliko amali za mja na tabu zake, na uhalisia nikuwa thawabu za Mwenyezi Mungu ni nyingi kuliko amali kwa kutazama namna na wingi wake.
Muumini huwa na dhana nzuri, na kutenda mema, na kwenda mbio na kuzidisha mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu.