Aina ndogo

Orodha ya Hadithi

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuyafanya mtu yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu kwake yeye.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu ameandika mema na mabaya kisha akalibainisha hilo, atakayepania kufanya jema kisha akawa hakulifanya analiandika Mwenyezi Mungu kwake jema kamili, na akilipania na akalifanya analiandika Mwenyezi Mungu kwake kuwa ni mema kumi mpaka kufikia ziada ya mia saba mpaka ziada nyingi zaidi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu hatazami katika mili yenu wala katika sura zenu, lakini anaangalia katika nyoyo zenu na matendo yenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Enyi waja wangu, Hakika mimi nimeharamisha dhulma katika nafsi yangu na nimeifanya kati yetu kuwa ni haramu hivyo msidhulumiane, Enyi waja wangu, nyinyi wote mmepotea ila yule niliyemuongoza niombeni uongofu nikuongozeni
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni watu wa ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Huteremka Mola wetu Aliyetakasika na kutukuka kila usiku katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho Anasema: Nani mwenye kuniita, nimjibu, nani mwenye kuniomba nimpe, nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) katika aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwasababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Amesema Mwenyezi Mungu -Mtukufu- mimi niko katika dhana ya mja wangu kwangu, na mimi niko pamoja naye pindi anaponikumbuka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hato msitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa atamsitiri Mwenyezi Mungu siku ya kiyama
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa