+ -

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضيَ اللهُ عنهما قَالَ:
قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِلْأَشَجِّ أَشَجِّ عَبْدِ الْقَيْسِ: «إِنَّ فِيكَ خَصْلَتَيْنِ يُحِبُّهُمَا اللهُ: الْحِلْمُ، وَالْأَنَاةُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 17]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema:
Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kumwambia Ashajji Abdil-Kaisi: "Hakika kwako wewe kuna mambo mawili anayapenda sana Mwenyezi Mungu: Upole, na utaratibu".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 17]

Ufafanuzi

Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kumwambia Mundhiri bin Aidhi, Ashajji ni kabila la Abdil-Kaisi na yeye ndiye alikuwa mtemi wao radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Hakika kwako kuna sifa mbili anazipenda mno Mwenyezi Mungu, nazo ni: Akili, kuhakiki mambo, na utulivu, na kutokuwa na pupa.

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kujipamba na upole utulivu.
  2. Himizo la kuhakiki mambo na kutazama mwisho wake.
  3. Upole na utaratibu ni miongoni mwa sifa nzuri.
  4. Mwenyezi Mungu Mtukufu humsifia mtu kwa sifa alizomuumba nazo miongoni mwa tabia njema.
  5. Ashajju: Ni mtu aliyejeruhiwa usoni, au kichwani, au katika paji la uso.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama