عن عائشة رضي الله عنها مرفوعاً: «إن المؤمن ليدرك بحسن خلقه درجة الصائم القائم»
[صحيح] - [رواه أبو داود وأحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakika muumini hufikia kwa tabia yake njema nafasi ya mfungaji mwenye kusimama usiku".
Sahihi - Imepokelewa na Abuu Daud
Ubora wa tabia njema, nakuwa huifikia mfanyaji wake nafasi nzuri mbele ya Mwenyezi Mungu na peponi nafasi ya mwenye kudumu katika swaumu na kusimama usiku, Na haya mawili ni mambo makubwa na ndani yake kuna tabu juu ya nafsi, na tabia njema ni jambo jepesi.