عن أنس بن مالك رضي الله عنه مرفوعاً: «إن الله ليرضى عن العبد أن يأكل الأكلة، فيحمده عليها، أو يشرب الشَّربة، فيحمده عليها».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...
Kutoka kwa Anas bin Maliki Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakika Mwenyezi Mungu huridhika kwa mja anapokula chochote, akamshukuru juu ya hicho, au akanywa chochote akamshukuru juu ya hicho".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim
Hakika katika sababu za kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kumshukuru juu ya kula na kunywa, kwani yeye Mtukufu peke yake, ndiye anayetoa fadhila kwa riziki hii.