عن عبد الله بن عمرو بن العاص - رضي الله عنهما- قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «إن المُقْسِطين عند الله على منابر من نور: الذين يعدلون في حكمهم وأهليهم وما ولَوُاْ».
[صحيح] - [رواه مسلم.
ملحوظة:
في صحيح مسلم زيادة على ما في رياض الصالحين: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إن المقسطين عند الله على منابر من نور، عن يمين الرحمن -عز وجل-، وكلتا يديه يمين»]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Hakika waadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika majukwaa ya nuru: wale wanaofanya uadilifu katika hukumu zao, na watu wao na yale waliyoyatawala".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim
Katika hadithi kuna habari njema kwa wale wanaohukumu kwa uadilifu baina ya watu ambao wako chini ya mamlaka yao na hukumu yao, nakuwa wao watakuwa juu ya majukwaa ya nuru ya uhakika kama takrima kwao siku ya kiyama mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.