عَنْ أَبِي حَازِمٍ قَالَ: قَاعَدْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ رضي الله عنه خَمْسَ سِنِينَ، فَسَمِعْتُهُ يُحَدِّثُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ:
«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لاَ نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ» قَالُوا: فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «فُوا بِبَيْعَةِ الأَوَّلِ فَالأَوَّلِ، أَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ، فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3455]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Haazim amesema: Nilikaa karibu na Abuu Huraira kwa muda wa miaka hamsini, nikamsikia akihadithia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema:
"Walikuwa wana wa Israeli wakiongozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii mwingine, na hakika hakuna nabii baada yangu, na watafuata Makhalifa (viongozi) baada yangu, na watakithiri" Wakasema: Unatuamrisha nini? Akasema: "Timizeni ahadi ya utiifu ya moja baada ya nyingine, wapeni haki zao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza walikuongozeni vipi".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3455]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa wana wa Israeli walikuwa wakiongozwa na Manabii, na wakisimamia mambo yao kama wanavyofanya viongozi na watawala kwa raia, kila unapodhihiri ufisadi Mwenyezi Mungu anawatumia Nabii kwa ajili ya kunyoosha mambo yao na kuondoa yale waliyoyabadilisha katika hukumu. Na hakika hakuna Nabii baada yangu ili afanye kama waliyokuwa wakiyafanya wale, na watakuja baada yangu watawala, na watakuwa wengi, na utatokea mzozano na kuhitilafiana baina yao. Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao wakamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Unatuamrisha tufanye nini? Akasema: Atakapochaguliwa kiongozi baada ya kiongozi; uteuzi wa kiongozi wa kwanza ndio uteuzi sahihi na ni wajibu kuutimiza na kuuheshimu, na uteuzi wa pili ni batili na ni haramu kwake kuukataa, na wapeni haki zao, na muwatii na muishi nao kwa usikivu na utii isipokuwa katika maasi, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza na atawahesabu kwa yale wanayokufanyieni.