عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «ما نهيتكم عنه فاجتنبوه، وما أمرتكم به فأْتُوا منه ما استطعتم، فإنما أَهلَكَ الذين من قبلكم كثرةُ مسائلهم واختلافهم على أنبيائهم».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi yaleteni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]
Ametuelekeza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake yakwamba yeye anapotukataza kitu ni wajibu kwetu kukiepuka bila kubagua, na akituamrisha chochote ni juu yetu kukifanya kwa kadiri tuwezavyo. Kisha akatutahadharisha ili tusijekuwa kama umma zilizotangulia pindi walipokithirisha maswali juu ya Manabii wao pamoja nakwenda kwao kinyume nao, akawaadhibu Mwenyezi Mungu kwa aina mbalimbali za maangamivu na adhabu, tunatakiwa tusiwe mfano wao ili tusiangamie kama walivyoangamia.