عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم:
«مَنْ أَحْدَثَ فِي أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ فِيهِ فَهُوَ رَدٌّ» متفق عليه.
ولمسلم: «مَنْ عَمِلَ عَمَلًا لَيْسَ عَلَيْهِ أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2697]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakayezua katika dini yetu hii, yale yasiyokuwemo, basi yatarejeshwa" Kaipokea Bukhari na Muslim. Na kutoka kwa Muslim: "Atakayefanya amali yoyote isiyokuwa na amri yetu, basi itarejeshwa".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2697]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetunga au kubuni jambo katika dini au akafanya amali yoyote ambayo haikuelekezwa na dalili yoyote kutoka katika Qur'ani na Sunna, basi jambo hilo litarejeshwa kwa mfanyaji wake na halitokubaliwa mbele ya Allah.