+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيَا نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ يَسَّرَ عَلَى مُعْسِرٍ يَسَّرَ اللهُ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا سَتَرَهُ اللهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَاللهُ فِي عَوْنِ الْعَبْدِ مَا كَانَ الْعَبْدُ فِي عَوْنِ أَخِيهِ، وَمَنْ سَلَكَ طَرِيقًا يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْمًا سَهَّلَ اللهُ لَهُ بِهِ طَرِيقًا إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إِلَّا نَزَلَتْ عَلَيْهِمِ السَّكِينَةُ، وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وَحَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ، وَذَكَرَهُمُ اللهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ، وَمَنْ بَطَّأَ بِهِ عَمَلُهُ لَمْ يُسْرِعْ بِهِ نَسَبُهُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2699]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamtatulia yeye tatizo katika matatizo ya siku ya Kiyama, na atakayemfanyia wepesi mwenye ugumu (katika jambo lake) Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi duniani na Akhera, na atakayemsitiri muislamu Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera, na Mwenyezi Mungu humsaidia mja pale mja anapokuwa katika kumsaidia ndugu yake, na atakayeshika njia akitafuta ndani yake elimu, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kupitia njia hiyo njia ya kuingia peponi, na hawajawahi kukusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakisomeshana baina yao, isipokuwa huwashukia utulivu na huwagubika rehema na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwataja (vizuri) kwa wale walioko kwake (Malaika), na yeyote ambaye matendo yake yatamchelewesha kuingia peponi basi ukoo wake hautompeleka mbio (kuingia)".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2699]

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa malipo ya muislamu mbele ya Mwenyezi Mungu ni kulingana na yale anayoyatenda muislamu pamoja na waislamu wenzake; atakayetatua na akafariji na akaondoa, na ampa nafuu muumini ya dhiki na tabu miongoni mwa shida za dunia, basi Mwenyezi Mungu atamlipa kwa kumtatulia tatizo miongoni mwa matatizo ya siku ya Kiyama. Na atakayemfanyia wepesi mwenye hali ngumu na akamrahisishia na akamuondolea ugumu wake, basi naye Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi katika dunia na Akhera. Na atakayemsitiri muislamu, kama akiyaona kwake yale yasiyofaa kudhihirishwa katika mapungufu na kuteleza, basi naye Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anakuwa mwenye kumsaidia mja wake, pale ambapo mja anapokwenda mbio kumsaidia ndugu yake katika masilahi yake ya dunia na Akhera, na msaada unakuwa kwa kumuombea dua, au kwa mwili na mali na mengineyo. Na atakayekwenda kwa ajili kutafuta elimu ya kisheria, akikusudia kupata radhi za Mwenyezi Mugnu Mtukufu; Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kwa elimu hiyo njia ya kuingia pepnoni. Na hawatojikusanya watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu, wakikisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakifundishana baina yao, isipokuwa huwateremkia utulivu na amani, na huwafunika na kuwaenea rehema ya Mwenyezi Mungu, na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwasifia kwa wale walio karibu kwake, na inatosha kuwa ni fahari kwa mja kutajwa na Mwenyezi Mungu kwa wale walioko juu. Na yatakayekuwa matendo yake ni pungufu, hayatomuunganisha na watu wenye vyeo kwa ajili ya matendo yao, anatakiwa asibweteke kwa utukufu wa nasaba na ubora wa baba zake, na akafanya uzembe katika amali.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Amesema bin Daqiiq Al-Idd: Hadithi hii ni tukufu mno, imekusanya aina mbali mbali za elimu na kanuni na adabu, ndani yake kuna fadhila za kukidhi haja za waislamu na kuwanufaisha kwa kadiri ya uwezo, kama elimu, au mali, au msaada, au kumuelekeza katika masilahi, na nasaha, au mengineyo.
  2. Himizo la kumfanyia wepesi mwenye hali ngumu.
  3. Himizo la kumsaidia mja muislamu, nakuwa Mwenyezi Mungu anamsaidia mwenye kusaidia kulingana na masada wake kwa ndugu yake.
  4. Miongoni mwa kumsitiri muislamu: Ni kutochunguza aibu zake, na imepokelewa kutoka kwa mmoja kati ya wema waliotangulia alisema kuwa: Niliishi na watu hawakuwa na aibu, waliposema aibu za watu, na watu wakasema aibu zao, na niliishi na watu hawakuwa na aibu, wakajizuia kuzungumza aibu za watu, zikasahaulika aibu zao.
  5. Si katika kuwasitiri watu kuacha uovu utendeke na kutoukemea, bali anaukemea na anasitiri, na hii ni kwa yule ambaye hajulikani kwa uovu na kuendelea katika ujeuri, na ama mwenye kufahamika kwa uovu, huyu hastahiki kusitiriwa, bali swala lake linafikishwa kwa mwenye mamlaka, kama hatohofia madhara kwa hilo; na hii ni kwa sababu kumsitiri kunamhadaa ili aendelee kuwaudhi watu, na anampa ujasiri mwingine katika watu wa shari na ukaidi.
  6. Himizo la kutafuta elimu na kusoma Qur'ani na kujifunza.
  7. Amesema Nawawi: Katika hili kuna dalili ya ubora wa kukusanyika katika kuisoma Qur'ani msikitini...na kunaunganishwa na msikiti katika fadhila hizi kukusanyika katika madrasa, na jihadi, na mfano wake, in shaa Allah.
  8. Malipo Mwenyezi Mungu ameyaweka katika matendo na si katika ukoo.