+ -

عن الْأَغَرِّ رضي الله عنه، وَكَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«يَا أَيُّهَا النَّاسُ تُوبُوا إِلَى اللهِ، فَإِنِّي أَتُوبُ فِي الْيَوْمِ إِلَيْهِ مِائَةَ مَرَّةٍ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2702]
المزيــد ...

Kutoka kwa Agharri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwa siku mara mia moja".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2702]

Ufafanuzi

Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu kukithirisha kuomba toba na msamaha, na anajielezea mwenyewe kuwa yeye hutubia kwa Mwneyezi Mungu Mtukufu na kumuomba msamaha kwa siku zaidi ya mara mia moja, na haliyakuwa alikwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, na katika hilo kuna ukamilifu wa kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kivetenamu Kikurdi Kireno Kiassam
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kila mmoja vyovyote itakavyokuwa nafasi yake na daraja lake katika imani, basi anahitaji kurejea kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kuikamilisha nafsi yake kwa toba, nakuwa kila mmoja hakosi mapungufu katika kutimiza haki za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: "Na tubieni kwa Mwenyezi Mungu nyote enyi waumini".
  2. Toba ni kwa mambo yote, sawa sawa kwa kufanya maharamisho au madhambi au uzembe katika kutimiza wajibu.
  3. Ikhlasi (kutakasa nia) katika toba ni sharti la kukubaliwa kwake, atakayeacha dhambi kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu huyo bado hajatubia.
  4. Amesema Nawawi: Toba ina masharti matatu: Ajivue katika maasi, na ajute kwa kuyafanya, na atie dhamira ya kweli ya kutorudi katika maasi mfano wake kabisa, na ikiwa maasi yanahusiana na haki ya binadamu basi kuna sharti la nne, nalo: Kurudisha haki aliyodhulumu kwa mwenye nayo, na kujivua nayo.
  5. Tahadhari: Kuomba msamaha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuna maana kuwa kuna madhambi aliyafanya, lakini ni kwa sababu ya ukamilifu wa utumwa wake na kufungamana kwake na kumtaja Aliyetakasika na kutukuka, na kuvuta kwake taswira ya utukufu wa haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na upungufu wa mja kwa namna yoyote atakayofanya katika kushukuru neema zake, nayo inakuwa ni sehemu ya kuwawekea sheria umma wake baada yake, na hukumu zinginezo.