عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم فيما يَحْكِي عن ربه تبارك وتعالى، قال: «أَذْنَبَ عَبْدٌ ذَنْبًا، فقال: اللهم اغْفِرْ لي ذَنْبِي، فقال اللهُ تبارك وتعالى: أَذْنَبَ عَبْدِي ذَنْبًا، فَعَلِمَ أَنَّ له رَبًّا يَغْفِرُ الذَّنْبَ، ويَأْخُذُ بالذَّنْبِ، ثم عَادَ فَأَذْنَبَ، فقال: أَيْ رَبِّ اغْفِرْ لي ذَنْبِي، فقال تبارك وتعالى: أَذْنَبَ عَبْدِي ذَنْبًا، فَعَلِمَ أَنَّ له رَبًّا، يَغْفِرُ الذَّنْبَ، ويَأْخُذُ بالذَّنْبِ، قَدْ غَفَرْتُ لِعَبْدِي فَلْيَفْعَلْ ما شَاءَ»
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- katika yale anayoyasimulia kutoka kwa Mola wake Aliyetakasika na kutukuka, Amesema: "Ametenda dhambi mja, akasema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi dhambi langu, akasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: Mja wangu katenda dhambi, na akajua kuwa ana Mola anayesamehe dhambi, na analichukua dhambi, kisha akarudia akatenda dhambi, na akasema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi dhambi langu, Akasema Aliyetakasika na kutukuka: Mja wangu katenda dhambi, na akajua kuwa ana Mola anayesamehe dhambi, na analichukua dhambi, basi hakika nimemsamehe mja wangu na afanye atakavyo".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Atakapofanya mja dhambi, kisha akasema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi dhambi langu, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: kafanya mja wangu dhambi, na akajua kuwa yeye ana Mola anayesamehe dhambi, akamsitiri na akaliachilia mbali, au akamuadhibu juu yake, kisha akarudi akatenda dhambi tena, Akasema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi dhambi langu, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: kafanya mja wangu dhambi, na akajua kuwa yeye ana Mola anayesamehe dhambi, akamsitiri na akaliachilia mbali, au akamuadhibu juu yake, basi hakika nimemsamehe mja wangu, basi na afanye ayatakayo katika madhambi na ayafuatishe na toba sahihi, madamu ataendelea kufanya hivi, anafanya dhambi anatubia ninamsamehe, kwani toba inabomoa yaliyo kabla yake.