+ -

عَن أَبِي بُرْدَةَ بْنِ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
وَجِعَ أَبُو مُوسَى وَجَعًا شَدِيدًا، فَغُشِيَ عَلَيْهِ وَرَأْسُهُ فِي حَجْرِ امْرَأَةٍ مِنْ أَهْلِهِ، فَلَمْ يَسْتَطِعْ أَنْ يَرُدَّ عَلَيْهَا شَيْئًا، فَلَمَّا أَفَاقَ، قَالَ: أَنَا بَرِيءٌ مِمَّنْ بَرِئَ مِنْهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَرِئَ مِنَ الصَّالِقَةِ وَالحَالِقَةِ وَالشَّاقَّةِ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1296]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Burda bin Abii Mussa radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Aliumia Abuu Mussa maumivu makali, akazimia na kichwa chake kikiwa katika paja la mwanamke katika wake zake, akawa hakuweza kumjibu chochote, alipozinduka, akasema: Mimi najitenga mbali na yule aliyejitenga mbali naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alijitenga mbali na mpiga mayowe, na mnyoa nywele, na mchana nguo.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1296]

Ufafanuzi

Amesimulia Abuu Burda radhi za Allah ziwe juu yake kuwa baba yake Abuu Mussa Al-Ash'ary radhi za Allah ziwe juu yake aliugua maradhi makali, akazimia, na kichwa chake kilikuwa katika paja la mwanamke mmoja katika wake zake, akapiga mayowe yule mwanamke kwa kumuita, akawa hakuweza kumjibu chochote kwa sababu ya kuzimia kwake. Alipozinduka akasema kuwa: Hakika yeye anajitenga mbali na yule aliyejitenga mbali naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alijitenga naye. Mpiga mayowe: Naye ni mwanamke anayenyanyua sauti yake wakati wa msiba. Na mnyoaji: Ni mwanamke anayenyoa nywele zake wakati wa msiba. Na mchana nguo: Ni mwanamke anayechana nguo zake wakati wa msiba. Kwa sababu haya ni katika mambo ya zama za ujinga, bali aliamrisha kuwa na subira wakati wa msiba, na kutaraji malipo yake kwa Mwenyezi Mungu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Katazo la kuchana nguo, na kunyoa nywele, na kunyanyua sauti wakati wa kutokea misiba, nakuwa hilo ni katika madhambi makubwa.
  2. Huzuni na kulia pasina maombolezo na kunyanyua sauti si haramu, hili halipingani na subira juu ya maamuzi ya Mwenyezi Mungu, bali ni rehema.
  3. Uharamu wa kulalamika katika makadirio ya Mwenyezi Mungu yenye kuumiza kwa kauli au vitendo.
  4. Uwajibu wa kuwa na subira wakati wa misiba.