+ -

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ أَكَلَ ثُومًا أَوْ بَصَلًا، فَلْيَعْتَزِلْنَا -أَوْ قَالَ: فَلْيَعْتَزِلْ- مَسْجِدَنَا، وَلْيَقْعُدْ فِي بَيْتِهِ»، وَأَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُتِيَ بِقِدْرٍ فِيهِ خَضِرَاتٌ مِنْ بُقُولٍ، فَوَجَدَ لَهَا رِيحًا، فَسَأَلَ فَأُخْبِرَ بِمَا فِيهَا مِنَ البُقُولِ، فَقَالَ قَرِّبُوهَا إِلَى بَعْضِ أَصْحَابِهِ كَانَ مَعَهُ، فَلَمَّا رَآهُ كَرِهَ أَكْلَهَا، قَالَ: «كُلْ فَإِنِّي أُنَاجِي مَنْ لاَ تُنَاجِي». ولِمُسْلِمٍ عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ أَكَلَ مِنْ هَذِهِ الْبَقْلَةِ، الثُّومِ - وقَالَ مَرَّةً: مَنْ أَكَلَ الْبَصَلَ وَالثُّومَ وَالْكُرَّاثَ فَلَا يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا، فَإِنَّ الْمَلَائِكَةَ تَتَأَذَّى مِمَّا يَتَأَذَّى مِنْهُ بَنُو آدَمَ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 855]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake", Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliletewa chungu kikiwa na mbogamboga, akakuta zinaharufu, akauliza akaelezwa kilichomo katika mboga hizo, akasema: Wapewe baadhi ya Maswahaba zake aliokuwa nao, alipoiona hakupendezwa nayo, akasema: "Kula kwani mimi ninanong'ona na yule usiyenong'ona naye".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 855]

Ufafanuzi

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekula kitunguu saumu au kitunguu maji asije msikitini, ili asiwaudhi ndugu zake katika wale wanaohudhuria swala ya jamaa kwa harufu yake, nalo ni katazo la kiusafi la kutokuja msikitini, na si katazo la kula; kwa sababu ni katika vyakula vya halali, na aliletewa Mtume rehema na amani ziwe juu yake chungu kikiwa na mbogamboga, aliponusa ndani yake harufu au alipoambiwa kilichomo, alikataa kula, na akakisogeza kwa baadhi ya Maswahaba zake akasema: Kula; kwani mimi husema na Malaika kwa wahyi.
Na akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hukereka na harufu mbaya, kama wanavyokereka watu kwa harufu hiyo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الرومانية Luqadda Oromaha
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Katazo la kuja msikitini kwa atakayekula kitunguu saumu, au kitunguu maji, au chochote chenye harufu mbaya.
  2. Inaunganishwa na mambo haya, kila chenye harufu mbaya kinachowakera wenye kuswali, kama harufu ya sigara na tumbaku ugoro na mfano wa hivyo.
  3. Sababu ya kukatazwa ni harufu, ikiondoka kwa kupikwa sana au kwa kinginecho; basi chukizo litaondoka.
  4. Chukizo la kula vitu hivi kwa mwenye ulazima wa kuhudhuria swala msikitni; ili jamaa isimpite msikitini, madam hajavila kwa hila ya kukwepa kuhudhuria swala ya jamaa, hapa itakuwa ni haramu.
  5. Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukataa kula kitunguu saumu na mfano wake, si kwa ajili ya kuharamisha, bali ni kwa sababu ya mazungumzo yake na Jibril amani iwe juu yake.
  6. Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba hukumu anaiambatanisha na sababu yake; ili mkusudiwa atulizane kwa kujua hekima.
  7. Amesema Al-qadhi: Na wanachuoni wametumia kipimo hiki kwa maeneo yote yanayowakusanya watu kwa ajili swala kama viwanja vya Idd na jeneza na mfano wake katika sehemu zinazowakusanya watu kwa ajili ya ibada, na vile vile sehemu wanazokusanyika kwa ajili ya elimu na kumtaja Mwenyezi Mungu na sherehe mbali mbali na mfano wake, isipokuwa masoko na mfano wake hayaingii hapa.
  8. Wamesema wanachuoni: Na katika hadithi hii kuna dalili ya kukataza kula kitunguu saumu na mfano wake wakati wa kuingia msikitini, hata kama pakiwa hakuna mtu ndani yake, kwa sababu ni mahala pa Malaika, na kwa ujumla wa maelekezo ya hadithi.