عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ غَدَا إِلَى الْمَسْجِدِ أَوْ رَاحَ أَعَدَّ اللهُ لَهُ فِي الْجَنَّةِ نُزُلًا، كُلَّمَا غَدَا أَوْ رَاحَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 669]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 669]
Amempa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kwenda msikitini kwa ajili ya ibada au elimu kwa lengo jingine katika mambo ya kheri katika wakati wowote; mwanzo wa mchana au mwisho wake kuwa Mwenyezi Mungu amemuandalia mahali na takrima ya ugeni peponi, kila anapokuja msikitini usiku au mchana.