+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«خَيْرُ صُفُوفِ الرِّجَالِ أَوَّلُهَا، وَشَرُّهَا آخِرُهَا، وَخَيْرُ صُفُوفِ النِّسَاءِ آخِرُهَا، وَشَرُّهَا أَوَّلُهَا».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 440]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Safu bora kwa wanaume ni safu ya kwanza, na safu yenye shari ni ya nyuma, na safu bora kwa wanawake ni safu ya mwisho na yenye shari ni safu ya mwanzo"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 440]

Ufafanuzi

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa safu bora kwa wanaume katika swala na yenye malipo makubwa na fadhila kubwa ni ya kwanza; kwakuwa watu wanakuwa karibu na imam na pia kusikiliza kisomo chake nakuwa kwao mbali na wanawake, na ya shari na yenye malipo na fadhila ndogo na iliyombali na matakwa ya sheria ni ya mwisho, na safu bora kwa wanawake ni safu ya mwisho; kwa sababu ndio inayowasitiri vizuri kwao, na iko mbali na kuchanganyikana na wanaume na macho yao na kufitinika nao, na safu ya shari ni ya kwanza; kwakuwa inakuwa karibu na wanaume na ni kujitia katika fitina.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الليتوانية الرومانية Luqadda malgaashka الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Amewahimiza wanaume kufanya haraka kwenda katika ibada mbalimbali na safu ya kwanza katika swala.
  2. Inafaa wanawake kuswali msikitini pamoja na wanaume katika safu zao binafsi, lakini kwa kujistiri na kujiheshimu.
  3. Wanawake wakikusanyika msikitini, basi wanatakiwa wapange safu, kama safu za wanaume, na wala wasitengane, bali wanatakiwa kushikana katika safu na kuziba nyufa, kama ilivyo katika safu za wanaume.
  4. Kumebainishwa namna sheria ilivyotilia umuhimu kwa kuhimiza kujiweka mbali wanawake na wanaume mpaka katika mahali pa ibada.
  5. Kutofautiana kwa watu ni kwa sababu ya matendo yao.
  6. Amesema Nawawi: Ama safu za wanaume kwa ujumla wake bora zaidi kuliko zote ni ile ya kwanza, na mbaya zaidi ni safu za mwisho, na ama safu za wanawake kilichokusudiwa katika hadithi ni: Safu za wanawake wanaoswali pamoja na wanaume, lakini wakiswali kwa peke yao na si pamoja na wanaume, basi hapo ni kama wanaume; safu yao bora zaidi ni safu ya kwanza na ya shari zaidi ni ya mwisho.
  7. Amesema Nawawi: Safu ya kwanza iliyosifiwa zikaja fadhila zake katika hadithi na kuihimiza ni safu inayofuata nyuma ya imam; sawa sawa mtu aje mapema au kwa kuchelewa, na sawa iwe kamili au pungufu na mfano wake au la.