+ -

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«أَتِمُّوا الصَّفَّ المُقَدَّمَ، ثُمَّ الَّذِي يَلِيهِ، فَمَا كَانَ مِنْ نَقْصٍ فَلْيَكُنْ فِي الصَّفِّ المُؤَخَّرِ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والنسائي] - [سنن أبي داود: 671]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Timizeni safu ya mbele, kisha inayofuata, na kama kuna mapungufu basi yawe katika safu ya mwisho".

[Sahihi] - [رواه أبو داود والنسائي] - [سنن أبي داود - 671]

Ufafanuzi

Amewaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanaume wenye kuswali kwa pamoja kukamilisha safu ya kwanza, kisha kukamilisha safu inayofuata, na kuendelea, na yakipatikana mapungufu katika safu basi yawe mapungufu haya katika safu ya mwisho.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa sunna katika kulinganisha sawa safu.
  2. Kwa wenye kuswali basi wasiache mapungufu katika safu ya mbele, bali yawe mapungufu katika safu ya nyuma.
Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kireno Thai Kiassam الهولندية الدرية المجرية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama