عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَوْ يَعْلَمُ النَّاسُ مَا فِي النِّدَاءِ وَالصَّفِّ الْأَوَّلِ ثُمَّ لَمْ يَجِدُوا إِلَّا أَنْ يَسْتَهِمُوا عَلَيْهِ لَاسْتَهَمُوا، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِي التَّهْجِيرِ لَاسْتَبَقُوا إِلَيْهِ، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِي الْعَتَمَةِ وَالصُّبْحِ لَأَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْوًا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 437]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Lau wangejua watu waliyomo katika Adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate nafasi ila kwa kupiga kura ili kuyafikia basi wangelipiga kura, na walau wangelijua yaliyomo katika kuwahi basi wangelishindana, na lau wangelijua yaliyomo katika swala ya usiku na swala ya Asubuhi, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 437]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba laiti watu wangelijua yaliyomo katika Adhana na safu ya kwanza miongoni mwa fadhila na kheri na baraka, kisha wakakosa namna ya kutangulizana na nani awe bora kuliko mwingine ila kwa kupiga kura, basi wangelipiga kura, na lau wangelijua yaliyomo katika kuwahi swala mwanzo wa wakati wake basi wangelishindana kuyaendea, na laiti wangelijua kiwango cha thawabu katika kuiendea swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, basi kungekuwa kwepesi kuziendea hata kwa kutambaa kwa magoti kama anavyotembea mtoto mwanzo wa kukua kwake.