+ -

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«تَابِعُوا بَيْنَ الحَجِّ وَالعُمْرَةِ، فَإِنَّهُمَا يَنْفِيَانِ الفَقْرَ وَالذُّنُوبَ كَمَا يَنْفِي الكِيرُ خَبَثَ الحَدِيدِ، وَالذَّهَبِ، وَالفِضَّةِ، وَلَيْسَ لِلْحَجَّةِ الْمَبْرُورَةِ ثَوَابٌ إِلاَّ الجَنَّةُ».

[صحيح] - [رواه الترمذي والنسائي وأحمد] - [سنن الترمذي: 810]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasikini na madhambi kama moto unavyoondoa uchafu wa chuma, na dhahabu, na fedha, na haina Hija nzuri na safi malipo isipokuwa Pepo".

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 810]

Ufafanuzi

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka karibu kati ya kutimiza ibada ya Hija na ibada ya Umra, na kutoacha kuzitekeleza hali yakuwa kuna uwezo, kwa sababu kuzitekeleza kwake inakuwa ni sababu ya kuondoa umasikini na madhambi na athari zake ndani ya moyo, kama ambavyo mpulizo wa moto huwa sababu ya kuondoa uchafu wa chuma na vyote vinavyochanganyika nacho katika madini ambayo si chuma.

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za kufuatanisha baina ya Hija na umra na himizo katika hilo.
  2. Kufuatanisha kati ya Hija na Umra ni miongoni mwa sababu za utajiri na msamaha wa madhambi.
  3. Amesema Al-Mubaarakafuriy: (Huondoa umasikini) Yaani: Huuondosha kabisa, na hii inategemea maana zote mbili: Umasikini unaoonekana kwa kupatikana utajiri wa mkononi, na umasikini wa ndani, kwa kupata utajiri wa moyo.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala Kivetenamu Kihausa Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama