عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنِينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا أَنَّهَا قَالَتْ:
يَا رَسُولَ اللَّهِ، نَرَى الجِهَادَ أَفْضَلَ العَمَلِ، أَفَلاَ نُجَاهِدُ؟ قَالَ: «لَا، لَكُنَّ أَفْضَلُ الجِهَادِ: حَجٌّ مَبْرُورٌ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 1520]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 1520]
Maswahaba Mwenyezi Mungu awawie radhi, waliona Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kupigana na maadui kuwa ni matendo bora, Basi Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akamuuliza Mtume Rehema na Amani zimshukie, je nao wapigane Jihadi?
Basi rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akawaelekeza kwenye Jihadi bora zaidi kwao, ambayo ni Hija iliyokubalika kwa mujibu wa Qur’ani na Sunna, isiyo na dhambi na unafiki (Riyaa).