+ -

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ:
قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِامْرَأَةٍ مِنَ الْأَنْصَارِ سَمَّاهَا ابْنُ عَبَّاسٍ فَنَسِيتُ اسْمَهَا: «مَا مَنَعَكِ أَنْ تَحُجِّي مَعَنَا؟» قَالَتْ: لَمْ يَكُنْ لَنَا إِلَّا نَاضِحَانِ فَحَجَّ أَبُو وَلَدِهَا وَابْنُهَا عَلَى نَاضِحٍ وَتَرَكَ لَنَا نَاضِحًا نَنْضِحُ عَلَيْهِ، قَالَ: «فَإِذَا جَاءَ رَمَضَانُ فَاعْتَمِرِي، فَإِنَّ عُمْرَةً فِيهِ تَعْدِلُ حَجَّةً».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1256]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema:
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia mwanamke mmoja miongoni mwa Ansari (Watu wa Madina) ambaye bin Abbas alimtaja kwa jina, lakini mimi nimelisahau jina lake: “Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi?” Akasema: Sisi tulikuwa na vilemba viwili tu, basi baba wa mwanawe na mwanawe walihiji kwa kilemba hicho na akatuachia kilemba kimoja ili tukifue.” Akasema: «Basi itakapokuja Ramadhani, basi fanya Umra, kwani Umra ndani ya Ramadhani ni sawa na Hija.”

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1256]

Ufafanuzi

Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, aliporejea kutoka katika Hija ya kuaga, alimwambia mwanamke mmoja wa Ansari ambaye hakuhiji: Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi?
Akatoa udhuru kwa sababu walikuwa na ngamia wawili, hivyo mume wake na mwanawe walihiji kwa mmoja wao, na kumwacha mwingine akichota maji kisimani.
Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, akamwambia kuwa kufanya Umra katika mwezi wa Ramadhani ni sawa na malipo ya Hija.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الدرية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za Umra ndani ya mwezi wa Ramadhani.
  2. Umra ndani ya Ramadhani inalingana sawa na Hija katika malipo, haina maana ya kuondosha uwajibu wa Hija.
  3. Malipo ya matendo huzidi kulingana na utukufu wa nyakati, ikiwemo matendo yanayofanywa ndani ya Ramadhani.