عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَتْ:
تُوُفِّيَتْ إِحْدَى بَنَاتِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَخَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «اغْسِلْنَهَا ثَلاَثًا، أَوْ خَمْسًا أَوْ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ، إِنْ رَأَيْتُنَّ بِمَاءٍ وَسِدْرٍ، وَاجْعَلْنَ فِي الآخِرَةِ كَافُورًا -أَوْ شَيْئًا مِنْ كَافُورٍ-، فَإِذَا فَرَغْتُنَّ فَآذِنَّنِي»، قَالَتْ: فَلَمَّا فَرَغْنَا آذَنَّاهُ، فَأَلْقَى إِلَيْنَا حِقْوَهُ، فَقَالَ: «أَشْعِرْنَهَا إِيَّاهُ»، وَقَالَتْ: وَجَعَلْنَا رَأْسَهَا ثَلاَثَةَ قُرُونٍ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1258]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema:
Alifariki mmoja kati ya mabinti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akatoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Muosheni mara tatu, au mara tano au zaidi ya hapo, mkiona kuna haja ya kuzidisha, kwa maji na mkunazi, na mwisho muweka kafuri -au chochote katika kafuri-, mkimaliza nipeni idhini" Anasema: tulipomaliza tulimpa idhini, akatupatia kikoi chake, akasema: "Mfunikeni kwa kikoi hiki", anasema: Na tukafanya (nywele za) kichwa chake kuwa mafungu matatu.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1258]
Alifariki Zainab binti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akaingia rehema na amani ziwe juu yake kwa wanawake waliotakiwa kumuosha, akasema: Muosheni kwa maji na Mkunazi kwa witiri mara tatu, au mara tano au zaidi ya hapo, ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo, na muweke katika muosho wa mwisho chochote katika kafuri, na mkimaliza nijulisheni. Walipomaliza kumuosha wakampa idhini, akawapa waoshaji kikoi chake, na akasema: Mzungushieni ndani yake na muifanye kuwa ndio nguo inayofuata mwili wake, kisha kikafanywa kichwa chake kuwa na mafungu matatu ya nywele.