عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: كان النبي صلى الله عليه وسلم يعتكف في كل رمضان عشرة أيام، فلما كان العام الذي قُبِضَ فيه اعتكف عشرين يوماً.
[صحيح] - [رواه البخاري]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akikaa itikafu katika kila ramadhani siku kumi, ulipofikia mwaka aliofishwa ndani yake alikaa itikafu siku ishirini
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akibakia msikitini akijitenga kwaajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu katika kila ramadhani siku kumi, na alikuwa akikaa itikafu katika siku kumi za katikati, kwa matarajio kuwa anaweza kuipata Lailatul Qadri (usiku wenye cheo), alipojua kuwa uko katika siku kumi za mwisho alikaa itikafu ndani ya siku hizo, kisha akakaa itikafu katika mwaka aliofishwa ndani yake siku ishirini kwa lengo la kuzidisha utiifu na kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo
Kuonyesha Tarjama
Ziyada