+ -

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَعْتَكِفُ العَشْرَ الأَوَاخِرَ مِنْ رَمَضَانَ، حَتَّى تَوَفَّاهُ اللَّهُ، ثُمَّ اعْتَكَفَ أَزْوَاجُهُ مِنْ بَعْدِهِ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2026]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu siku kumi za mwisho wa Ramadhani, mpaka alimpomfisha Mwenyezi Mungu, kisha wakakaa itikafu wake zake baada yake.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2026]

Ufafanuzi

Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alidumu na itikafu katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, kwa ajili ya kuutafuta usiku wenye cheo (Lailatul-Qadri), na akaendelea katika hilo mpaka Mwenyezi Mungu alipomfisha, na wakadumu na itikafu wake zake baada yake, radhi za Allah ziwe juu yao.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sheria ya kukaa itikafu misikitini, hata kwa wanawake kwa kuzingatia vigezo vya kisheria, na kwa sharti la kuwa na amani dhidi ya fitina.
  2. Inakuwa na mkazo itikafu katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani kwa kudumu nazo Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Itikafu ni sunna endelevu wala haikufutwa, kwani walikaa itikafu wake zake Mtume rehema na amani ziwe juu yake baada yake.