+ -

عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
تَسَحَّرْنَا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، ثُمَّ قَامَ إِلَى الصَّلاةِ، قُلْتُ: كَمْ كَانَ بَيْنَ الأَذَانِ وَالسَّحُورِ؟ قَالَ: قَدْرُ خَمْسِينَ آيَةً.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1921]
المزيــد ...

Kutoka kwa Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Tulikula daku pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha akasimama kwenda katika swala, nikasema: Ulipita muda gani baina ya adhana na daku? Akasema: Kiasi cha (kusoma) aya hamsini.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1921]

Ufafanuzi

Walikula daku baadhi ya Maswahaba pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha akasimama rehema na amani ziwe juu yake kwenda katika swala ya Alfajiri. Anasi akasema kumuuliza Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake: Kulikuwa na kiwango cha muda gani baina ya adhana na kumaliza kula daku?. Akasema Zaidi radhi za Allah ziwe juu yake: Kiasi cha kusoma aya hamsini za kati na kati, si ndefu wala fupi, wala si kwa kisomo cha haraka wala cha taratibu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الرومانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ubora wa kuchelewesha daku mpaka kabla kidogo na Alfajiri; kwa sababu ikichelewa kunakuwa na manufaa katika mwili, na manufaa yake kwake mchana ni mengi.
  2. Pupa ya Maswahaba ya kukusanyika pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili wajifunze kutoka kwake.
  3. Uzuri wa maisha ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Maswahaba zake, kiasi kwamba alikuwa akila pamoja nao.
  4. Wakati wa kujizuia kula ni kuchomoza kwa Alfajiri.
  5. Kauli yake: "Kulikuwa na muda gani baina ya adhana na daku", makusudio yake ni kati ya daku na kukimiwa swala, kwa kauli yake ndani ya hadihti nyingine: "Kulipita muda gani baina ya kumaliza kwao kula daku na kuingia katika swala", na hadithi hujifasiri zenyewe.
  6. Amesema Muhallab: Hapa kuna kukadiria nyakati kwa matendo ya mwili, na waarabu walikuwa wakikadiria wakati kwa matendo, kama kusema kwao: Kiasi cha kumkamua mbuzi, na kiasi cha kumchinja ngamia mnene, Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake akaachana na hayo, akaenda kukadiria muda kwa kisomo cha Qur'ani; Akiashiria kuwa wakati huo ulikuwa ni wakati wa ibada ya kisomo, na lau kama wangelikuwa wakikadiria muda kwa kingine kisichokuwa matendo basi angesema kwa mfano: Kiasi cha daraja moja, au theluthi ya tano ya saa.
  7. Amesema bin Abii Jamra: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitazama ni lipi litakalokuwa na huruma zaidi kwa umma wake basi analifanya; kwa sababu lau kama asingelikula daku basi wangelimfuata, na lingewapa tabu baadhi yao, na lau angelikula daku usiku wa manane pia hilo lingewapa tabu baadhi yao miongoni mwa wale wanaozidiwa na usingizi, kwani hilo linaweza kupelekea mtu kuacha kuswali swala ya Alfajiri au akahitaji nguvu kubwa ya kukesha.