عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ:
كُنَّا نُخْرِجُ إِذْ كَانَ فِينَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ، عَنْ كُلِّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ، حُرٍّ أَوْ مَمْلُوكٍ، صَاعًا مِنْ طَعَامٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ أَقِطٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ زَبِيبٍ، فَلَمْ نَزَلْ نُخْرِجُهُ حَتَّى قَدِمَ عَلَيْنَا مُعَاوِيَةُ بْنُ أَبِي سُفْيَانَ رضي الله عنه حَاجًّا، أَوْ مُعْتَمِرًا فَكَلَّمَ النَّاسَ عَلَى الْمِنْبَرِ، فَكَانَ فِيمَا كَلَّمَ بِهِ النَّاسَ أَنْ قَالَ: إِنِّي أَرَى أَنَّ مُدَّيْنِ مِنْ سَمْرَاءِ الشَّامِ، تَعْدِلُ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، فَأَخَذَ النَّاسُ بِذَلِكَ، قَالَ أَبُو سَعِيدٍ: فَأَمَّا أَنَا فَلَا أَزَالُ أُخْرِجُهُ كَمَا كُنْتُ أُخْرِجُهُ، أَبَدًا مَا عِشْتُ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 985]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Kudry -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Tulikuwa tukitoa kipindi alipokuwa nasi Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul fitiri, kwa kila mdogo na mkubwa, huru au mamluki, kibaba cha chakula, au kibaba cha siyagi, au kibaba cha ngano, au kibaba cha zabibu, hatukuacha kuendelea kuitoa, mpaka alipokuja kwetu Muawia bin Abii Sufian radhi za Allah ziwe juu yake kwa ajili ya Hija, au Umra, akazungumza na watu katika Mimbari, ikawa katika yale aliyozungumza na watu alisema kuwa: Hakika mimi ninaona kuwa vibaba viwili vya kipimo cha kutoka Samraa ya Sham, vinalingana na kibaba kimoja cha tende, watu wakalichukua hilo, anasema Abuu Saidi: Ama mimi niliendelea kuitoa kama nilivyokuwa nikiitoa, milele kwa muda wote nilioishi.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 985]
Waislamu walikuwa wakitoa zakatul-fitiri katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na zama za makhalifa waongofu baada yake kwa mdogo na mkubwa, kiwango cha kibaba cha chakula. Na chakula chao kilikuwa ni ngano na (Zabibu): Zabibu kavu, na (samli): Maziwa yaliyokaushwa na tende. Na kiwango cha kibaba kimoja ni 'mudi' nne, na mudi moja inalingana na ujazo wa viganja viwili vya mtu aliyelingana sawa. Alipokuja Muawia radhi za Allah ziwe juu yake katika mji wa Madina akiwa Khalifa, na ngano ya Sham ilikuwa nyingi wakati huo, alitoa hotuba akasema: Hakika mimi ninaona vibaba viwili vya ngano ya Sham (ni nusu ya kibaba), vinalingana na nusu ya kibaba cha tende, watu wakalichukua hilo. Akasema Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake: Ama mimi ninaendelea kutoa kama nilivyokuwa nikitoa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake daima maishani mwangu.