عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ:
فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الفِطْرِ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، عَلَى العَبْدِ وَالحُرِّ، وَالذَّكَرِ وَالأُنْثَى، وَالصَّغِيرِ وَالكَبِيرِ مِنَ المُسْلِمِينَ، وَأَمَرَ بِهَا أَنْ تُؤَدَّى قَبْلَ خُرُوجِ النَّاسِ إِلَى الصَّلاَةِ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1503]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema:
Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kibaba cha ngano, kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1503]
Amewajibisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri baada ya Ramadhani, nayo kwa kiwango cha kibaba inafikia uzito wake machoto manne. Na mudi moja: Ni ujazo wa viganja viwili vya mtu wa kati na kati, wa tende au ngano, kwa kila muislamu; aliye huru na mtumwa, mwanaume na mwanamke, mdogo na mkubwa, na hii ni kwa yule ambaye anachakula kinachozidi kwa siku yake hiyo na usiku wake, kwake yeye na kwa wale anaowahudumia. Na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala ya Iddi.