+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَا تَقَدَّمُوا رَمَضَانَ بِصَوْمِ يَوْمٍ وَلَا يَوْمَيْنِ إِلَّا رَجُلٌ كَانَ يَصُومُ صَوْمًا فَلْيَصُمْهُ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1082]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Msiitangulizie Ramadhani kwa swaumu ya siku moja wala siku mbili, isipokuwa mtu aliyekuwa akifunga swaumu fulani basi na aifunge".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1082]

Ufafanuzi

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kufunga kabla ya Ramadhani kwa siku moja au siku mbili, kwa nia ya kuchukua tahadhari kuwa huenda Ramadhani imeingia; kwa sababu ulazima wa Ramadhani umewekwa katika kuonekana kwa mwandamo, na wala hakuna haja ya kujikalifisha, isipokuwa kama mtu alikuwa akifunga swaumu aliyoizoea, kama kufunga siku moja na kula siku moja, au siku ya juma tatu na Alhamisi ikaangukia siku hiyo basi na afunge; na wala hilo halihesabiki kuwa ni katika kuipokea Ramadhani, na inaunganishwa hapo swaumu zitakazokuwa za wajibu kama kulipa deni na swaumu ya nadhiri.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Katazo la kujilazimisha, na uwajibu wa kuzihifadhi ibada kama zilivyowekwa na sheria pasina kuzidisha au kupunguza.
  2. Miongoni mwa hekima za hilo -na Allah ndiye mjuzi zaidi- ni kutofautisha kati ya ibada za faradhi na sunna, na kujiandaa kwa Ramadhani kwa uchangamfu na shauku, na ili swaumu iwe ndiyo nembo ya mwezi mtukufu yenye kujipambanua nayo.
Ziada