عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُما قَالَ:
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ، فَرَأَى زِحَامًا وَرَجُلًا قَدْ ظُلِّلَ عَلَيْهِ، فَقَالَ: «مَا هَذَا؟»، فَقَالُوا: صَائِمٌ، فَقَالَ: «لَيْسَ مِنَ البِرِّ الصَّوْمُ فِي السَّفَرِ»، وَفِي لَفْظٍ لِمُسلِمٍ: «عَلَيْكُمْ بِرُخْصَةِ اللهِ الَّذِي رَخَّصَ لَكُمْ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1946]
المزيــد ...
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao amesema:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona msongamano na mtu kazingirwa, akasema: "Nini hicho?", wakasema: Alikuwa kafunga swaumu, akasema: "Si katika wema kufunga safarini", na katika tamko la Muslim: "Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1946]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona mtu mmoja watu wamemkusanyikia na wamemzingira ili kumkinga na joto la jua na wingi wa kiu, akasema: Kapatwa na nini? Wakasema: Anaswaumu, akasema: Si katika wema kufunga safarini, Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni.