+ -

عن أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«تَسَحَّرُوا، فَإِنَّ فِي السَّحُورِ بَرَكَةً».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1923]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Chelewesheni kula daku, hakika katika kuchelewesha kula daku kuna baraka".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1923]

Ufafanuzi

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kula daku, nako ni kula mwisho wa usiku ili kujiandaa kwa ajili ya swaumu; kwa sababu ndani yake kuna baraka, na kheri nyingi, yakiwemo malipo na thawabu, na kusimama katika wakati wa mwisho kwa ajili ya kuomba dua, na kupata nguvu kwa ajili ya swaumu, na kupata uchangamfu kwa ajili yake, na kupunguza uzito wake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sunna ya kula daku na kutekeleza amri ya sheria kwa kufanya hivyo.
  2. Amesema bin Hajari katika kitabu Fat-hulbaari: Baraka katika daku zinapatikana kwa namna nyingi: Nayo ni kufuata sunna na kwenda kinyume na Mayahudi na Wakristo, na kupata nguvu kutokana na daku kwa ajili ya ibada, na kuongeza uchangamfu, na kuondoa tabia mbaya inayosababishwa na njaa, na kuwa sababu ya kutoa sadaka kwa mwenye kuomba kwa wakati huo, au akajumuika pamoja naye katika chakula, na ni sababu ya kufanya dhikri na dua katika wakati ambao kuna matarajio makubwa ya kujibiwa, na kuipata nia ya kufunga kwa yule aliyejisahau kabla ya kulala.
  3. Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba alikuwa akioanisha hukumu kwa hukumu; ili mioyo ya watu ikunjuke, na ujulikane utukufu wa sheria.
  4. Amesema bin Hajari: Daku inapatikana kwa chochote kidogo atakachokula mtu, katika vyakula au vinywaji.