عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَا يَزَالُ النَّاسُ بِخَيْرٍ مَا عَجَّلُوا الْفِطْرَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1098]
المزيــد ...
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Wanaendelea watu kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1098]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa watu wataendelea kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu ndani ya Ramadhani baada kuhakiki kuzama kwa Jua; na hii ni kwa sababu ya kutekeleza sunna, na kusimama katika mpaka wake.