عَنْ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا:
أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: أَرَأَيْتَ إِذَا صَلَّيْتُ المَكْتُوبَاتِ، وَصُمْتُ رَمَضَانَ، وَأَحْلَلْتُ الحَلَالَ، وَحَرَّمْتُ الحَرَامَ، وَلَمْ أَزِدْ عَلَى ذَلِكَ شَيْئًا، أَأَدْخُلُ الجَنَّةَ؟ قَالَ: «نَعَمْ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [الأربعون النووية: 22]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Abdillaah Jabiri bin Abdillah Al-Aswari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao:
Kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-akasema: "Waonaje ikiwa nitaswali swala zilizofaradhishwa, na nikafunga Ramadhani, na nikahalalisha kilichokuwa halali na nikaharamisha kilichokuwa haramu, na wala sikuzidisha zaidi ya hayo je nitaingia peponi?Akasema: "Ndiyo".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [الأربعون النووية - 22]
Anaweka wazi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayeswali swala tano zilizofaradhishwa na wala hakuzidisha zaidi ya hizo swala tano kwa kuswali swala za Sunna, na akafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na akawacha kufunga funga za sunna, na akaamini uhalali wa vilivyo halali na akavitekeleza na akaamini uharamu wa vilivyo haramu na akajiepusha navyo, kwa hakika mtu huyo ataingia Peponi.