Aina:
+ -


____

[] - []
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Amri - na inasemekana ni Abuu Amra, Sufiani bin Abdillah radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema:
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [الأربعون النووية - 21]

Ufafanuzi

Swahaba Sufiani bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amfundishe kauli iliyokusanya maana nzima ya Uislamu ili ashikamane nayo na wala hatomuuliza yeyote zaidi yake? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Sema: Nimempwekesha Mwenyezi Mungu, na nimemuamini kuwa yeye ndiye Mola wangu na Mungu wangu na Muumba wangu na muabudiwa wangu wa haki aisye na mshirika wake, kisha awe mtiifu katika sheria za Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza faradhi za Mwenyezi Mungu na kuacha maharamisho ya Mwenyezi Mungu na adumu katika hilo.

Katika Faida za Hadithi

  1. Msingi wa Dini ni kumuamini Mwenyezi Mungu kwa Ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake.
  2. Umuhimu wa kuwa na msimamo baada ya kuamini, na kudumu na ibada na kuthubutu juu ya hilo.
  3. Imani ni sharti la kukubaliwa matendo.
  4. Kumuamini Mwenyezi Mungu kunakusanya yote yanayopaswa kuitakidi miongoni mwa itikadi za imani na misingi yake, na yanayofuata hilo miongoni mwa amali za moyo, na kutii na kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa siri na kwa wazi.
  5. Msimamo ni kubaki katika njia, kwa kutekeleza wajibu na kuacha makatazo.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka الفولانية Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga اليونانية الأكانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية الخميرية الماراثية
Kuonyesha Tarjama
Aina tofauti
Ziada