____
[] - []
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Masoud Uqba ni Amri Al-Answari Al-Badri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu:
"Hakika katika yale waliyoyakuta watu miongoni mwa maneno ya kiutume ya mwanzo, usipokuwa na haya basi fanya ulitakalo".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [الأربعون النووية - 20]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika yale yaliyokuja na usia ndani yake kutoka kwa Manabii waliotangulia, na yakaenea kwa watu na watu wakarithishana kutoka kwao karne baada ya karne, mpaka yakamfikia wa mwanzo katika umma huu, ni; tazama unayotaka kuyafanya, ikiwa yatakuwa ni katika mambo ambayo si aibu basi fanya, na ikiwa ni katika mambo ya aibu basi acha; kwa sababu kinachozuia kufanya matendo mabaya ni haya, atakayekosa aibu basi hutumbukia katika kila machafu na maovu.