____
[] - []
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Abdirahman Abdallah bin Omari bin Khattwab radhi za Mweneyzi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".
[Sahihi] - [رواه البخاري ومسلم] - [الأربعون النووية - 3]
Ameufananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Uislamu na jengo madhubuti kwa nguzo zake tano zenye kulibeba jengo hilo, na mambo mengine ya Uislamu kama nyenzo zenye kulikamilisha jengo hilo, Na nguzo ya kwanza katika nguzo hizo ni: Shahada mbili; Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hizo mbili ni nguzo moja; kila moja haitengani na nyingine, mja anazitamka kwa kukiri umoja wa Mwenyezi Mungu na kustahiki kwake kuabudiwa yeye pekee pasina mwingine, na kufanyia kazi makusudio ya nguzo hii, na kwa kuamini utume wa Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumfuata yeye. Na nguzo ya pili: Ni kusimamisha swala, nazo ni swala tano za faradhi usiku na mchana: Alfajiri, Adhuhuri, lasiri, Maghribi, na Ishaa, kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake. Na nguzo ya tatu: Ni kutoa zaka ya lazima, nayo ni ibada ya mali ya wajibu katika kila mali iliyofikia kiwango maalumu katika sheria, ambayo hupewa wastahiki wake. Na nguzo ya nne: Ni Hija, nayo nikutia nia ya kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada, kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. Na nguzo ya tano: Ni kufunga mwezi wa Ramadhani, nako ni kujizuia na kula na kunywa na vinginevyo miongoni mwa vyenye kufunguza kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuzama jua.