عن ابن عباس رضي الله عنهما : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم لما بعث معاذا إلى اليمن قال له: "إنك تأتي قوما من أهل الكتاب، فليكن أولَ ما تدعوهم إليه شهادة أن لا إله إلا الله" -وفي رواية: "إلى أن يوحدوا الله-، فإن هم أطاعوك لذلك فأعلمهم أن الله افترض عليهم خمس صلوات في كل يوم وليلة، فإن هم أطاعوك لذلك فأعلمهم أن الله افترض عليهم صدقة تؤخذ من أغنيائهم فَتُرَدُّ على فقرائهم، فإن هم أطاعوك لذلك فإياك وكَرَائِمَ أموالِهم، واتق دعوة المظلوم فإنه ليس بينها وبين الله حجاب".
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ibn Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yakwamba Mtume rehema na Amani zimfikie alipomtuma Mua'dhi kwenda Yemen alisema kumwambia: "Hakika wewe unawaendea watu waliopewa kitabu, basi naliwe jambo la mwanzo utakalowaita kwalo ni kushuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu" na katika riwaya nyingine "Mpaka wampwekeshe Mwenyezi Mungu-, ikiwa wao watakutii katika hilo, basi wajulishe kuwa Mwenyezi Mungu amewafaradhishia juu yao swala tano katika kila usiku na mchana, ikiwa wao watakutii kwa hilo, basi wajulishe kuwa Mwenyezi Mungu amewafaradhishia juu yao sadaka, zinachukuliwa kutoka kwa matajiri wao, na kurejeshwa kwa masikini wao,ikiwa wao watakutii kwa hilo, basi tahadhari na mali zao za thamani, na ogopa sana maombi ya mwenye kudhulumiwa, kwani hayo hayana kati yake na Mwenyezi Mungu kizuizi".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Nikuwa Mtume rehema na Amani zimfikie alipomuelekeza Muadhi bin Jabali radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie kwenda katika nchi ya Yemen kama mlinganizi (muhubiri) na Mwalimu, alimchorea mikakati ambayo atapitia katika ufikishaji wake, akamuweka wazi kuwa yeye atakutana na watu wenye elimu na mijadala miongoni mwa mayahudi na wakristo, ili awe na maandalizi ya kujadiliana nao na kujibu hoja zao, kisha aanze katika ufikishaji wake kwa jambo la Muhimu zaidi kisha linalofuata, awaite kurekebisha itikadi kwanza; kwasababu ndio msingi, wakilitii hilo awaamrishe kusimamisha swala, kwasababu ndio wajibu mkubwa baada ya Tauhidi, ikiwa wataisimamisha awaamrishe matajiri wao kutoa zaka za mali zao kuwapa mafukara wao, kwaajili ya kuwaliwaza na kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, kisha akamtahadharisha na kutochukua mali nzuri; kwasababu ya wajibu ni ya kati na kati, kisha akamuhimiza juu ya uadilifu na kuacha dhulma; ili aliyedhulumiwa asijekumuombea dua mbaya na dua yake ni yenye kupokelewa.