عَن عَبدِ الله بنِ الشِّخِّير رضي الله عنه قَالَ:
انْطَلَقْتُ في وَفدِ بَنِي عَامِرٍ إِلى رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقُلنا: أَنتَ سيّدُنَا، فقال: «السَّيدُ اللهُ»، قُلنا: وَأَفْضَلُنا فَضْلاً، وأعظَمُنا طَوْلاً، فقال: «قُولُوا بِقَولِكُم، أَو بَعضِ قولِكُم، وَلَا يَسْتَجْرِيَنَّكُم الشَّيطَانُ».
[صحيح] - [رواه أبو داود وأحمد] - [سنن أبي داود: 4806]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Shikhiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Nilisafiri katika msafara wa Bani Aamir kwenda kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Tukasema: Wewe ni bwana yetu, akasema: "Bwana ni Mwenyezi Mungu", Tukasema: Na mbora zaidi kuliko sisi katika fadhila, na mtoaji zaidi kuliko sisi, akasema: "Semeni kwa maneno mliyozoea, au baadhi yake, na wala asikukokoteni Shetani".
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 4806]
Lilikuja kundi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, walipofika kwake wakasema -kwa kumsifu- kwa baadhi ya maneno ambayo aliyachukia -Rehema na amani ziwe juu yake-, Wakasema: "Wewe ni bwana yetu", Akasema kuwaambia -Rehema na amani ziwe juu yake- "Bwana ni Mwenyezi Mungu" Yeye ndiye mwenye ubwana uliokamilika juu ya viumbe wake nao ni waja wake. Na wakasema: "Wewe ndiye mbora wetu" na mwenye daraja na utukufu wa juu kuliko sisi na mwenye sifa nyingi. Na wewe "Ndiye mtoaji zaidi kuliko sisi" na mwingi wa ukarimu na utukufu na daraja ya juu. Kisha akawaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake waseme kauli yao iliyozoeleka na wasijilazimishe kutafuta maneno mengine, na kuwa shetani asiwavute katika kuchupa mipaka na kupitiliza kunakopelekea kuingia katika yale yaliyoharamishwa miongoni mwa shirki na njia zake.