+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم أنه قال:
«وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَا يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هَذِهِ الْأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلَا نَصْرَانِيٌّ، ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلَّا كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ».

[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- amesema:
"Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni".

Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Anaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna atayemsikia katika umma huu, Myahudi au Mkristo au mwingine yeyote utakayemfikia ujumbe wa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- kisha akafa na hakumuamini isipokuwa atakuwa miongoni mwa watu wa motoni ataishi humo milele daima.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الغوجاراتية القيرقيزية النيبالية اليوروبا الليتوانية الدرية الصومالية الكينياروندا
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuenea kwa ujumbe wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa ulimwengu mzima, na ulazima wa kumfuata kwake, na kufutwa kwa sheria zote kupitia sheria yake.
  2. Atakayempinga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hayatomfaa kitu madai yake ya kudai kumwamini Nabii mwingine katika Manabii -Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao wote-.
  3. Ambaye hakumsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na haukumfikia ujumbe wa Uislamu huyu atapewa udhuru, na hukumu yake huko Akhera itakuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Yanathibitika manufaa kwa Uislamu kwa mtu hata kama atasilimu muda mchache kabla ya kifo, hata kama atakuwa katika maradhi mabaya, madama tu roho haijafika kooni.
  5. Kuiona kuwa ni sahihi dini ya makafiri -wakiwemo Mayahudi na Wakristo- ni ukafiri.
  6. Amemtaja Myahudi na Mkristo katika hadithi kama tahadhari kwa wenye kuwaona kuwa wako sawa; na hii ni kwakuwa Mayahudi na Wakristo wana kitabu, na ikiwa ndio hivyo, basi kwa wengine wasiokuwa na kitabu ndio wanastahiki zaidi kuingia motoni, wote hao wanalazimika kuingia katika dini yake na kumtii yeye Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.