+ -

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«كُلُّ أُمَّتِي يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَنْ أَبَى»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، وَمَنْ يَأْبَى؟ قَالَ: «مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أَبَى».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 7280]
المزيــد ...

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni nani atakaye kataa? Akasema: "Atakaye nitii ataingia peponi, na atakaye niasi atakuwa amekataa".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 7280]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba umma wake wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa!.
Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- wakasema: Ni nani atakaye kataa ewe Mjumbe wa Allah?!
Akawajibu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa atakayejisalimisha na akafuata na akamtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ataingia peponi, na ama atakaye asi na akawa hakujisalimisha katika sheria atakuwa kakataa mwenyewe kuingia peponi kwa sababu ya matendo yake mabaya.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka الفولانية Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Nikuwa kumtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kumuasi kwake ni sehemu ya kumuasi Mwenyezi Mungu.
  2. Kumtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hupelekea kuipata pepo, na kumuasi kwake kunapelekea kuingia motoni.
  3. Habari njema kwa watiifu walioko katika umma huu, nakuwa wote wataingia peponi isipokuwa atakayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
  4. Huruma yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa umma wake, na pupa yake katika kuwaongoa.