+ -

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ:
كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا دَخَلَ الْعَشْرُ أَحْيَا اللَّيْلَ، وَأَيْقَظَ أَهْلَهُ، وَجَدَّ وَشَدَّ الْمِئْزَرَ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1174]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
"Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi (za mwisho wa ramadhani) anauhuisha usiku, na anawaamsha watu wake, na anaongeza juhudi na anakaza kikoi".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1174]

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi za mwisho wa ramadhani anauhuisha usiku wote kwa aina mbali mbali za ibada, na anawaamsha familia yake kwa ajili ya swala, na anajitahidi katika ibada zaidi ya kawaida yake, na anajitenga kwa ajili yake na anajitenga na wake zake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo na kufaidika na nyakati bora kwa matendo mema.
  2. Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii: Nikuwa inapendeza kuzidisha katika ibada mbali mbali katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, na kupendeza kuhuisha siku zake kwa ibada mbali mbali.
  3. Yampasa kila mja awe na pupa kwa familia yake ya kuwaamrisha kufanya ibada, na awe mvumilivu juu yao.
  4. Kufanya mambo ya heri kunahitaji uthubutu na subira na kuvumilia.
  5. Amesema Nawawi: Wametofautiana wanachuoni katika maana ya (Kukaza kikoi) wakasema: Ni kuongeza juhudi katika ibada zaidi ya kawaida yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika nyakati zingine, na maana yake: Ni kujipinda katika ibada, husemwa: Jambo hili nimelifungia kikoi, yaani: Nimelidhamiria na nimetenga muda wangu kwa ajili yake, na wamesema wengine: Ni fumbo la kujitenga na wanawake kwa ajili ya kushughulika na ibada.