عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا:
أَنَّ رِجَالًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُرُوا لَيْلَةَ القَدْرِ فِي المَنَامِ فِي السَّبْعِ الأَوَاخِرِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَرَى رُؤْيَاكُمْ قَدْ تَوَاطَأَتْ فِي السَّبْعِ الأَوَاخِرِ، فَمَنْ كَانَ مُتَحَرِّيهَا فَلْيَتَحَرَّهَا فِي السَّبْعِ الأَوَاخِرِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2015]
المزيــد ...
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-:
Yakwamba kuna baadhi ya watu katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, walionyeshwa Lailatul qadri ndotoni katika siku saba za mwisho wa Ramadhani. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Naona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho, basi atakayetaka kuitafuta basi na aitafute katika siku saba za mwisho".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2015]
Wanaume katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake waliona ndotoni kuwa Lailatul Qadri inakuwa katika siku saba za mwisho wa Ramadhani. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ninaona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho wa Ramadhani, atakayeitaka, akiwa na pupa ya kuitafuta, basi ajitahidi kuiwinda na kuitafuta kwa kukithirisha matendo mema kwani inatarajiwa zaidi kuwa katika siku saba za mwisho, nazo zinaanza kwanzia usiku wa tarehe ishirini na nne mwezi wa Ramadhani unapokuwa na siku thelathini, na zinaanza usiku wa tarehe thelathini na tatu mwezi unapokuwa wa siku ishirini na tisa.