عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«تَحَرَّوْا لَيْلَةَ القَدْرِ فِي الوِتْرِ مِنَ العَشْرِ الأَوَاخِرِ مِنْ رَمَضَانَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2017]
المزيــد ...
Na imepokelewa kutoka kwa Aisha -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Utafuteni usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) katika witiri za kumi la mwisho katika Ramadhani".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2017]
Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufanya juhudi kuutafuta usiku wenye cheo kwa kuzidisha amali njema, nao hutarajiwa zaidi kupatikana katika siku za witiri za siku kumi za mwisho wa Ramadhani kila mwaka, nazo ni: Ishirini na moja, na ishirini na tatu, na ishirini na tano, na ishirini na saba, na ishirini na tisa.