عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
أَوْصَانِي خَلِيلِي صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِثَلاَثٍ: صِيَامِ ثَلاَثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ، وَرَكْعَتَيِ الضُّحَى، وَأَنْ أُوتِرَ قَبْلَ أَنْ أَنَامَ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1981]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
"Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga siku tatu katika kila mwezi, na rakaa mbili baada ya kuchomoza jua (Dhuhaa), na nisali witiri kabla sijalala".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1981]
Anaeleza Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa kipenzi chake na jamaa yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuusia na akamsisitizia mambo matatu:
La kwanza: Kufunga siku tatu katika kila mwezi.
La pili: Rakaa mbili za Dhuhaa kila siku.
La tatu: Kusali witiri kabla ya kulala; na hii ni kwa mtu atakayehofia kutoamka mwisho wa usiku.