+ -

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا:
أَنَّ تَلْبِيَةَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَبَّيْكَ اللهُمَّ، لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ، إِنَّ الْحَمْدَ وَالنِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ» قَالَ: وَكَانَ عَبْدُ اللهِ بْنُ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا يَزِيدُ فِيهَا: لَبَّيْكَ لَبَّيْكَ، وَسَعْدَيْكَ، وَالْخَيْرُ بِيَدَيْكَ، لَبَّيْكَ وَالرَّغْبَاءُ إِلَيْكَ وَالْعَمَلُ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1184]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-:
"Nikuwa Talbiya (kuitika) kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kulikuwa ni: Labbaikallaahumma labbaika -Nimekuitikia ewe Mola nimekutikia, Labbaika laa shariika laka labbaika -Nimekuitikia huna mshirika wako nimekuitikia, Hakika sifa njema na neema zote ni zako pamoja na ufalme, wewe pekee usiye na mshirika.". Amesema: Na alikuwa Abdallah bin Omari akizidisha ndani yake: "Labbaika Labbaika wasa'daika, -Nimekuitikia nimekuitikia na utukufu ni wako, wal khairu biyadaika, -Na heri iko mikono mwako, na hamu zote na matendo mwisho ni kwako".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1184]

Ufafanuzi

Zilikuwa talbiya (kuitika katika Hija) kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuingia katika ibada ya Hija au Umra ni kusema: "Nimekuitikia ewe mola nimekuitikia" Kuitika kwa lazima kwako baada kukuitikia katika yale uliyotuita kwayo miongoni mwa ikhlasi na tauhidi na Hija na mengineyo, "Nimekuitikia, huna mshirika wako, nimekuitikia" wewe peke yako ndiye unayestahiki kuabudiwa huna mshirika wako katika uumbaji wako na uungu wako na majina yako na sifa zako, "hakika sifa njema" na shukurani na sifa "na neema" zinatoka kwako, na wewe ndiye mgawaji wake "ni zako" hugawanywa katika kila hali, "na ufalme" vile vile ni wako, "huna mshirika wako" wote ni wako wewe peke yako. Na alikuwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao akizidisha katika hayo. "Labbaika wasa'daika" Nimekuitikia na utukufu ni wako, nifurahishe kwa furaha moja baada ya nyingine, "na heri iko mikononi mwako" yote, na ni kwa fadhila zako, "Nimekuitikia na shauku zote ziko kwako" na matakwa na maombi ninayaelekeza kwa yule ambaye heri iko mkononi mwake, "na matendo" ni kwa ajili yako, kwani wewe ndiye unayestahiki kuabudiwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sheria ya kuleta talbiya (muitikio) katika Hija na Umra, na mkazo wake ndani yake; kwa sababu hiyo ndiyo nembo yake maalumu, kama ambavyo takbiri (Allaahu Akbar) ni nembo ya swala.
  2. Amesema bin Munir: Na katika sheria ya talbiya kuna ukumbusho juu ya ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake kuwa misafara yao kwenda katika Al-kaaba ilikuwa ni kwa wito maalum kutoka kwake Aliyetakasika na kutukuka.
  3. Kilicho bora ni kushikamana na talbiya ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hakuna tatizo kuongeza, kwa kukiri kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hilo, amesema bin Hajari: Na hii ndio namna ya uadilifu zaidi, kwa kusema pekee maneno yalikuja kwa kuchukuliwa moja kwa moja kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akichagua kauli iliyokuja kutoka kwa swahaba pekee, au akaanzisha mwenyewe katika yale yanayofaa, yeye mwenyewe peke yake ili maneno yasichanganyike na yale yaliyonukuliwa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hii inafanana na hali ya dua katika tahiyatu, kwani alisema katika dua hiyo: Kisha achague katika maombi na sifa azitakazo: Yaani baada ya kumaliza ile iliyofundishwa.
  4. Sunna ya kunyanyua sauti katika talbiya, na hii ni kwa wanaume, ama mwanamke atashusha sauti yake kwa kuhofia fitina.
Ziada