+ -

عَنْ أَبِي عُبَيْدٍ، مَوْلَى ابْنِ أَزْهَرَ، قَالَ:
شَهِدْتُ العِيدَ مَعَ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، فَقَالَ: هَذَانِ يَوْمَانِ نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ صِيَامِهِمَا: يَوْمُ فِطْرِكُمْ مِنْ صِيَامِكُمْ، وَاليَوْمُ الآخَرُ تَأْكُلُونَ فِيهِ مِنْ نُسُكِكُمْ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1990]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Ubaidi, mwachwa huru wa bin Azhari, amesema:
Nilishuhudia swala ya Idd pamoja na Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Siku mbili hizi alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga ndani yake: Siku ya kufungua kwenu kutoka katika swaumu yenu, na siku nyingine ni ile mnayokula katika vichinjwa vyenu.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1990]

Ufafanuzi

Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga siku ya Iddil-Fitiri na Iddil-Adh-ha; ama Iddil-Fitiri ni siku ya kufungua kutoka katika swaumu ya mwezi wa Ramadhani, na ama Iddil-Adh-ha ni siku ya kula katika vichinjwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa kufunga siku mbili za Iddil-Fitiri na Iddil-Adh-ha, na siku tatu za kubanika nyama; kwa sababu zinafuatana na siku ya Iddil-Adh-ha isipokuwa kwa yule ambaye hakupata cha kutoa, itafaa kwake kufunga siku za kubanika nyama.
  2. Amesema bin Hajari: Imesemekana kuwa: Na faida ya kuzitaja siku mbili ni ishara ya kuonyesha sababu ya uwajibu wa kufungua ndani yake, nazo ndio mapumziko ya swaumu, na kudhihirisha ukamilifu wake peke yake kwa kufungua siku zilizo baada yake, na Idd nyingine ni kwa ajili ya kuchinja kwa mwenye kujikurubisha kwa kichinjwa chake ili ale kutoka katika kichinjwa hicho.
  3. Inapendeza kwa mtoa hotuba ataje katika hotuba yake yale yanayohusiana na wakati wake miongoni mwa hukumu, na atumie fursa ya matukio kama hayo.
  4. Sheria ya kula kutoka katika kichinjwa cha ibada.
Ziada