عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ نَسِيَ وَهُوَ صَائِمٌ، فَأَكَلَ أَوْ شَرِبَ، فَلْيُتِمَّ صَوْمَهُ، فَإِنَّمَا أَطْعَمَهُ اللهُ وَسَقَاهُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1155]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyezi Mungu kamlisha na kamnywesha".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1155]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekula au kunywa kwa kusahau akiwa kafunga swaumu ya faradhi au sunna basi atimize swaumu yake wala asifungue; kwa sababu hakukusudia kufungua, bali hiyo ni riziki Mwenyezi Mungu kamsogezea na akamlisha na kumnywesha.