عن أبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَا يَحِلُّ لِامْرَأَةٍ مُسْلِمَةٍ تُسَافِرُ مَسِيرَةَ لَيْلَةٍ إِلَّا وَمَعَهَا رَجُلٌ ذُو حُرْمَةٍ مِنْهَا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1339]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Si halali kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja, isipokuwa awe pamoja na mwanaume mwenye uharamu wa kumuoa (ndugu yake)".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1339]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni haramu kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja isipokuwa awe pamoja na mwanaume katika maharimu wake.